Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge laishauri NEC kuwawajibisha wasimamizi wanapofanya uzembe

50526 BUNGE+PIC

Fri, 5 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria imeishauri Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufuatilia wasimamizi wake wa uchaguzi na kuwawajibisha pale wanapofanya uzembe.

Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Najma Giga ameyasema hayo bungeni leo wakati akisoma maoni ya kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2018/19 pamoja na makadirio na mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu kwa mwaka wa fedha 2019/20.

“Kamati inaendelea kuishauri Tume ya Taifa ya Uchaguzi ihakikishe inafuatilia wasimamizi wake wa uchaguzi na kuwawajibisha pale wanapofanya uzembe  unaosababisha madhara ambayo yangeweza kudhibitiwa mapema na msimamizi aliye makini na anayetambua na kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria,” amesema. 

Amesema kamati hiyo pia inaishauri Serikali kutoa fedha zilizoidhinishwa na Bunge kwa wakati ili kuiwezesha Nec kuratibu masuala mbalimbali ya uchaguzi kwa ufanisi.

Giga amesema kamati hiyo inaendelea pia kuishauri NEC kufanya kazi yake kwa weledi ili kuendelea kuaminika kwa wadau wake wa uchaguzi.

“Hii ni pamoja na kuhakikisha kwamba inawashirikisha wadau wa uchaguzi wakati wa uhuishaji wa daftari la wapiga kura ili kuepuka migogoro isiyokuwa na tija,” amesema.



Chanzo: mwananchi.co.tz