Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge lahairishwa kufuatia kifo cha Mbunge ACT Wazalendo

86c6b9d7e3491d9754fe28473e4c1fd4 Bunge lahairishwa kufuatia kifo cha Mbunge ACT Wazalendo

Thu, 20 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeahirisha vikao vyake vya leo mpaka kesho kufuatia kifo cha Mbunge wa jimbo la Konde kupitia Chama cha ACT Wazalendo Khatib Haji, aliyefariki dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Akitoa taarifa ya msiba huo mapema leo Mei 20, 2021, Bungeni Dodoma, Naibu Spika wa Bunge hilo Dk Tulia Ackson, amesema kuwa mbunge huyo amefariki wakati akipatiwa matibabu na mazishi yanafanyika leo saa 10:00 jioni huko visiwani Pemba.

"Mheshimiwa Spika kwa masikitiko makubwa anawatangazia waheshimiwa wabunge kwamba mbunge mwenzetu Khatib Haji, mbunge wa jimbo la Konde kupitia Chama cha ACT Wazalendo, amefarikia dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili na mazishi yatafanyika leo Pemba, tutawakilishwa na wabunge wenzetu walioko Dar es Salaam", ameeleza Dk Tulia

Chanzo: www.habarileo.co.tz