Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge la wananchi Chadema wachaguana

CHADEMAPIC 660x400 Bunge la wananchi Chadema wachaguana

Fri, 16 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa waliokuwa wagombea ubunge kupitia Chadema katika uchaguzi wa mwaka 2020 wanaounda Bunge la Wananchi wamefanya uchaguzi wa Spika na Naibu Spika.

Uchaguzi huo unafanyika kufuatia semina ya siku mbili iliyofunguliwa jana Desema 14, 2022 na Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika na unatarajiwa kufungwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe leo Desemaba 15, 2022.

Mwandishi wa Mwananchi anayefuatilia uchaguzi huo ameshuhudia makada hao wakiendelea na uchaguzi.

Baada ya uchaguzi mkuu 2020 Chadema kupitia Baraza Kuu kiliridhia kuanzisha kwa chombo ili kuweza kuwasemea wananchi nje ya bunge baada ya kushinda jimbo moja.

"Katika kikao cha Kamati Kuu kilichokutana Septemba mwaka huu miongoni mwa mambo tuliyokubalana ni pamoja na kuanza mikutano ya hadhara.

"Kafanyeni maandalizi kwenye maeneo yenu na kutoa taarifa ili chama kiweze kuanza mikutano hiyo, kwani ni wajibu kwa vyombo vyote vya chama kuanzia ngazi ya Kanda na mabara kufanya maandalizi ili tujue lini tunaanza," amesema Mnyika wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live