Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge Lajadili Malori Kukwama Bandarini Dar

Bunge 3?fit=700%2C467&ssl=1 Bunge Lajadili Malori Kukwama Bandarini Dar

Thu, 13 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Bunge Lajadili Malori Kukwama Bandarini Dar May 13, 2021 by Global Publishers



Bunge la Tanzania limeahirisha mjadala wa Wizara ya Afya kwa takribani nusu saa ili kujadili sakata la malori kutoshusha wala kupakia mizigo kwa muda wa siku tano katika Bandari ya Dar es Salaam.

Hoja ya kuahirishwa kwa mjadala imewasilishwa jana Jumatano Mei 12, 2021 na mbunge wa Mafinga Mjini (CCM), Cosato Chumi.

Chumi amesema Bandari hiyo ndio chanzo kikubwa cha kuendeleza nchi na kufanikisha miradi, “malori hayashushi wala kupakia mizigo kwa maana uchumi kwa namna fulani umesimama. Na tunazungumzia ushindani kati ya bandari yetu na nchi jirani.”

“Katika hali hii hatuwezi kukaa kimya na kuacha mambo ya namna hii yaendelee ndio maana ninajenga hoja tuahirishe mjadala ili tujadili jambo hili nyeti.”

Amesema kuna mizigo inayokwenda kwenye miradi mbalimbali ikiwemo wa uzalishaji wa umeme wa maji katika bwawa la mwalimu Nyerere na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), lakini imekwama katika bandari hiyo.

Amesema mizigo inayokwenda nchi jirani imekwama wakati Taifa linatarajia bandari hiyo kuwa na ushindani. Baada ya hoja hiyo, Naibu Spika Dk Tulia Ackson aliruhusu hoja hiyo ijadiliwe kwa muda wa dakika 20 ambapo wabunge saba walipata nafasi ya kuchangia.

Akijibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema tayari Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekwenda Dar es Salaam kushughulikia suala hilo.

Chanzo: globalpublishers.co.tz