Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge: Askofu Gwajima Asimamishwe

GWAJIMA2?fit=1280%2C720&ssl=1 Bunge: Askofu Gwajima Asimamishwe

Tue, 31 Aug 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Kamati ya Bunge imetoa azimio sakata la Mbunge wa Jimbo la Kawe, Josephat Gwajima kupewa adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili mfululizo ya Bunge.

Akiwasilisha ripoti ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka Bungeni amesema;

“Kamati imebaini kauli za Mhe. Gwajima zinadhalilisha nafasi ya Mbunge na kushusha heshima ya Bunge, wabunge na viongozi, zinachonganisha mhimili wa bunge dhidi ya Serikali na wananchi, zinaonyesha dharau na kushusha heshima ya bunge na uongozi wa Bunge.” Mwakasaka, M/Kiti Kamati

MAONI YA KAMATI YA BUNGE

“1. Vyombo vya kisheria vifuatilie mwenendo na vitendo vya Askofu Josephat Mathias Gwajima kutokana na kauli mbalimbali alizotoa kwani zinaashiria  kuwepo na jinai na uvunjifu wa amani na usalama wan chi.

“2. Suala hili lishughulikiwe kwa mujibu wa sheria na maadili ya umma, lifikishwe kwenye chama anachotoka, ili aweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni za chama chake,” amesema Mwakasaka.

MAAZIMIO YA BUNGE

“Bunge linaazimia kwamba, Mhe. Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe apewe adhabu ya kutohudhuria Mikutano miwili mfululizo ya Bunge baada ya kupitishwa ka azimio hili.” – Emmanuel Mwakasaka, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maadili.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati Gwajima alifanya makosa hayo kati ya tarehe zifuatazo; 25 Julai, 01 Agosti  15 Agosti, 21 Agosti.

Chanzo: globalpublishers.co.tz