Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunda wamlilia Kinana ahadi hewa za viongozi

Bunda Wamlilia Kinana Ahadi Hewa Za Viongozi Bunda wamlilia Kinana ahadi hewa za viongozi

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulurahman Kinana amekea tabia ya viongozi wa serikali ambao wamekuwa na tabia ya kutoa ahadi ambazo wanajua wazi hazitekelezeki au mipango yake haipo ili kuepuka malalamiko ya wananchi.

Kinana ametoa karipio hilo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Bunda Mjini wilayani Bunda mkoani Mara ambapo wananchi walilalamika Serikali iliwataka wahame katika maeneo yao kupisha ujenzi wa mradi wa maendeleo na tathimini ilifanyika lakini hadi sasa hawaelewi hatima yao na hawatakiwi kuendeleza maeneo hayo.

Pia wananchi hao wameonesha kukerwa na kitendo cha maeneo yao kuchukuliwa na nyumba zao kubomolewa pamoja na kupewa masharti ya kutofanya shughuli zozote za kimaendeleo katika maeneo hayo likiwemo eneo la Kijiji cha Nyantwate.

Akizungumza katika mkutano huo mwananchi wa Kijiji cha Nyantwale, Saasita Mchanga amesema wanateswa na ahadi ya serikali iliyowataka kuhama eneo hilo lakini mpaka sasa hawajalipwa fidia huku wananyimwa kulima na kufanya shughuli nyingine za maendeleo akitolea mfano wanashindwa kujenga matundu ya choo katika shule yao kwa kusuburi hatma yao ili wahame.

"Shule yetu inazaidi ya wanafunzi 200 na wanauhaba wa matundu ya vyoo, kwa sasa kuna matundu mawili pekee, sasa tunahofu tunaweza kupata magonjwa ya mlipuko," amesema Kutokana na malalamiko hayo Kinana alionesha kukasirishwa na kuwataka viongozi wa Wilaya ya Bunda kufikiria nje ya boksi na kwamba wanazuia eneo ili kuweka uwekezaji wa EPZA wakati hawana uhakika kama wawekezaji watakuja kuwekeza.

“EPZA ya Dar es Salaam mpaka sasa haijaja, mwekezaji gani atakuja kuwekeza huku Bunda, yaani mmezuia eneo kwa miaka 15 kwa ajili ya uwekezaji ambao hamjui hata Wapakistani watakuja lini……

Viongozi mmepewa dhamana mnatakiwa mfikirie nje ya boksi, wekeni uwekezaji unaowazunguka huku kuna samaki kwa nini msiweke viwanda vya samaki, viwanda vya pamba, mnahodhi eneo kuendeleza hamuendelezi, mmewanyang’anya wananchi alafu hakuna kitu chochote kinachofanyika limekaa tu mmebaki kutoa ahadi ambazo hazitekelezeki," Amesisitiza Kinana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live