Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bulaya "Mafunzo ya silaha JKT wasipewe wote"

Screenshot 2021 03 31 At 13.58.13 660x400.png Bulaya "Mafunzo ya silaha JKT wasipewe wote"

Thu, 1 Apr 2021 Chanzo: millardayo.com

Mbunge wa Viti Maalum, Ester Bulaya, ametoa wito kwa Serikali kutoa mafunzo ya kutumia silaha kwa Vijana wachache wanaoshiriki mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) badala ya kuwafundisha wengi.

Bulaya amesema kutoa mafunzo ya silaha kwa Vijana wengi wakati hawapati nafasi za kujiunga na Jeshi hilo inaweza kupelekea baadhi yao kutumia mafunzo waliyopata kufanya uhalifu.

Aidha, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa, amesema Jeshi hutoa mafunzo ya silaha kwa Vijana katika idadi inayotakiwa na mafunzo ya JKT yanalenga kuwajengea Vijana uwezo wa kujitegemea badala ya kuajiriwa.

DK. MPANGO ALIVYOPIGWA NA BUTWAA BAADA YA JINA LAKE KUTAJWA KUWA MAKAMU WA RAIS

Chanzo: millardayo.com