Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking: Mzee Mangula aomba kung'atuka, Kinana kupewa mikoba

Mangula Kinana Breaking: Mangula aomba kung'atuka, Kinana kupewa mikoba

Thu, 31 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Mzee Philip Japhet Mangula leo Alhamisi Machi 31,2022 amewasilisha barua kwenye Halmashauri kuu ya

CCM akiomba kuachia ngazi nafasi yake hiyo.

Aidha, Kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM kimependekeza jina la Katibu Mkuu wa zamani wa chama hicho, Abdulrahman Kinana kuteuliwa kupigiwa kura za kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Bara ambapo atachukua nafasi ya Mzee Philip Mangula. Kikao hicho kimefanyika leo Machi 31, 2022 Jijini Dodoma.

Updates:

Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana leo amepitishwa na Kikao Cha Halmashauri Kuu ya Taifa-CCM kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi Philip Mangula kuandika barua ya kuachia nafasi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live