Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking: Mbunge Khatib Haji Afariki Dunia

Mbunge?fit=645%2C367&ssl=1 Breaking: Mbunge Khatib Haji Afariki Dunia

Thu, 20 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

MBUNGE wa Jimbo la Konde, kisiwani Pemba, Khatib Haji wa Chama cha ACT Wazalendo, amefariki Dunia. Umauti umemfika katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili akipatiwa matibabu Alfajiri ya leo, Alhamisi, Mei 20, 2021.

Khatibu aliwahi kuwa Mbunge wa Konde kupitia Chama cha Wananchi CUF mwaka 2010 hadi 2020. Alishawahi kushika nafasi ya Waziri wa Kilimo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mwaka 1984 hadi 1987.

Katika Bunge hili la 12, Khatib amekuwa Mbunge wa tatu kufariki tangu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. January 21 2021 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Martha Umbulla alifariki dunia na Februari 12, 2021 Mbunge wa Jimbo la Muhambwe, Mkoa wa Kigoma Atashasta Nditiye alifariki Dunia baada ya kupata ajali ya gari.

Chanzo: globalpublishers.co.tz