Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking: Bernard Membe arejeshwa CCM

Membe Ccm Membe

Thu, 31 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa imemsamehe na kumrudishia uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwanasiasa na Mwanadiplomsia Mkongwe, Bernard Camilius Membe aliyekuwa amefukuzwa ndani ya CCM.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Machi 31, 2022 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka imeeleza kuwa Ndugu Membe ameandika barua ya kuomba msamaha kwa zaidi ya mara tatu.

Membe ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, alifukuzwa uanachama Februari 2020 kwa makosa ya kinidhamu na baadae akagombea Urais kupitia ACT-Wazalendo.

Katika Kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika leo Machi 31, 2022 Jijini Dodoma, kimeamua kuwa Membe na wengine ambao wamerejeshewa uanachama wao watakabidhiwa kadi zao maeneo waliyopo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live