Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi ATCL aikubali ripoti ya CAG

52155 PIC+ATCL

Mon, 15 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi amesema kilichoelezwa katika ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali ndiyo uhalisia wa mwenendo wa shirika hilo.

Jana akizungumza na Mwananchi, hata hivyo, Matindi alisema kwa sasa kuna mabadiliko chanya katika ukuaji kibiashara na mwenendo wa shirika hilo kutokana na hatua zilizochukuliwa kulifufua.

Ripoti ya CAG iliyotolewa mapema wiki hii ilisema mashirika 14 ya umma yanamatatizo ya kifedha na hasara hadi kusababisha madeni zaidi ya mitaji yao ikiwamo ATCL.

Matindi alisema shirika hilo limepunguza kiwango cha hasara kukoka Sh38.72 bilioni mwaka 2005/2006 hadi Sh16.21 mwaka 2016/2017.

“Hasara imepunguza mtaji wa shirika mpaka kufikia mtaji hasi. Kwa miaka mitatu ya karibuni nimeanza kuona mwenendo mzuri wa shirika maana hasara imepungua kwa asilimia 58,” alisema ripoti ya CAG.

Ripoti hiyo ilisema kupungua kwa hasara hiyo kumetokana na kuongezeka kwa mapato ya shirika hilo kwa asilimia 20 na kupunguza gharama ya uendeshaji kwa asilimia 27.

Related Content

Akifafanua, Matindi alisema kupungua kwa hasara hiyo kunatokana na hatua kadhaa zilizochukuliwa za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuwa na adabu katika manunuzi yanayofanywa.

“Tumeondoa safari za wafanyazi zisizo za lazima hivi sasa tunaruhusu safari ambazo zina tija katika ukuaji wa biashara ya shirika vilevile katika manunuzi tumeondoa utaratibu wa mtu kufanya manunuzi kwa masilahi yake na kujiongezea ‘percent’ alisema Matindi ambaye shirika analoliongoza kulingana na mpango wake wa biashara linatarajia kuacha kupata hasara ifikapo mwaka 2023 na kwamba ripoti ya CAG ni wakati walikuwa na ndege mbili pekee, lakini sasa kuna ukuaji mkubwa zaidi baada ya ujio wa ndege nyingine mbili (Bomberdier Q400 na Boeing 787 Dreamliner) zinazotarajiwa Novemba mwaka huu biashara itashamili zaidi. Kwa sasa ATCL ina ndege nane.



Chanzo: mwananchi.co.tz