Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Boniface, Malisa wafikishwa Mahakama ya Kisutu

Boniface Meya Kisutu.png Boniface, Malisa wafikishwa Mahakama ya Kisutu

Mon, 6 May 2024 Chanzo: mwanachidigital

Meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob na mwanaharakati, Godlisten Malisa, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashtaka matatu ya kuchapisha taarifa za uongo kinyume na sheria.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo leo Mei 6, 2024 na kusomewa mashtaka yao na wakili wa Serikali, Neema Moshi akishirikiana na Happy Mwakanyamale, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ushindi Swallo.

Wakili Moshi amesemaa wameshatakiwa chini ya kifungu cha 16 cha sheria ya Makosa ya Kimtandao namba 14 ya mwaka 2015.

Akiwasomea mashtaka yao, Moshi amedai kuwa washtakiwa wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 11805/2024.

Chanzo: mwanachidigital