Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodaboda watakiwa kuwalinda wanafunzi wa kike

Bodaboda Watakiwa Kuwalinda Wanafunzi Wa Kike Bodaboda watakiwa kuwalinda wanafunzi wa kike

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Katibu Mkuu umoja wa vijana CCM Taifa (UVCCM) Mussa Peter Mwakitinya amewataka madereva wa usafirisha (boda boda) kuhakikisha wanawalinda wanafunzi wa kike lengo hili waweze kutimiza ndoto zao katika masomo.

Ameyasema hayo yote wakati Akizungumza na Madereva wa boda boda. Katika tarafa ya Vunta Mamba wilayani Same katika jimbo la Same Mashariki kuelekea kwenye sherehe ya uzinduzi wa Samia Cup 2023 ambayo yameandaliwa na Mh. Mbuge wa jimbo hilo Anne Kilango.

Hivyo. Nitumie fulsa hii kuongea na ndugu zangu (bodaboda) kuachana na tabia ya mafataki kuwarubuni wabinti wadogo na wanafunzi kikubwa kuwa walinzi wa wadogo zetu wakike maana Serikali inatambua Kazi kubwa Inayo fanywa na vijana hivyo niwaombe Madereva wa (bodaboda) kuwa mabalozi wazuri katika kuleta Maendeleo na kuakikisha mnawalinda wanafunzi dhidi ya ukatili wa kijinsia Amesema MNEC Mwakitinya

Niwaombe ndugu zangu wa bodaboda endeleeni kuchapa kazi katika jimbo letu la Same Mashariki hii Kazi ni kama kazi nyingine tumeona bodaboda wengi wanafanikiwa katika Maisha kujenga nyumba nzuri na kusomesha watoto kupitia Kazi hiyo sambamba na hayo tuendelee kumuunga Mkono Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na Mbuge Anne Kilango anawathamini Sana ndugu zangu wa jimbo la Same Mashariki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live