Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodaboda, magari yaupamba msafara wa Lowassa kuelekea Monduli

Bodaboda, magari yaupamba msafara wa Lowassa kuelekea Monduli

Mon, 11 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Msafara wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye alitangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) Machi 1, 2019 ukiwa na magari na pikipiki zaidi 100 umeanza safari kuelekea wilayani Monduli mkoani Arusha ili kukabidhiwa kadi ya CCM.

Lowassa amewasili katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha saa 6.20 mchana na kupokewa na viongozi wa CCM wakiongozwa na mjumbe wa NEC taifa, Daniel Awaki na baada ya hapo alipumzika katika chumba cha wageni mashuhuri (VIP) kabla ya kuanza safari ya kwenda Monduli.

Tofauti na wakati mwingine anapopata fursa, huzungumza na wanahabari Lowassa aliwapungia mkono watu waliofika uwanjani hapo na kuingia kwenye gari kuanza safari.

Hata  hivyo, msafara huo ulioongozwa na makada wa CCM  ulitawaliwa na mbwembwe za kila aina kutoka kwa waendesha bodaboda na magari.

Tofauti za wakati mwingine,  leo polisi hawakuwepo kuongoza magari na njiani makada wa CCM walikuwa wamesimama wakimsalimia Lowassa.

Safari ya kwenda Monduli ambapo atakabidhiwa kadi ya CCM inatarajiwa kuchukua saa moja.

Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kinachojiri kutoka Monduli



Chanzo: mwananchi.co.tz