Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bavicha wakosoa sherehe za uhuru kufutwa wakiwa Segerea

30834 Bavicha+pic Mwenyekiti wa  Bavicha Patrick Olesosopi

Mon, 10 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baraza la vijana chadema  wameadhimisha siku ya Uhuru kwa kuwatembelea viongozi wa chama hicho walioko gereza la Segerea huku wakikosoa uamuzi wa kufutwa kwa sherehe hizo.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Muweka hazina wa  Baraza la  Wanawake la chama hicho Ester Matiko wako gereza la Segerea kwa siku ya 14 baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana Novemba 26.

Akizungumza leo  Desemba 9, Mwenyekiti wa  Bavicha Patrick Olesosopi amesema siku ya Uhuru ni muhimu kwa Taifa katika kuwakumbuka waasisi waliolipigania Taifa hili.

"Baada ya kufutwa kwa sherehe za Uhuru sisi kama Bavicha kwa pamoja tuliazimia kujitokeza katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kutembelea watu alionyimwa waliokosa Uhuru" amesema Sosopi.

Amesema kwa kuwa sherehe za Uhuru ni muhimu, Rais angeangalia sherehe nyingine za kufuta ikiwamo kupunguza siku za kukimbiza mwenge ili kuokoa fedha ambazo matumizi yake sio ya lazima lakini sio siku ya uhuru.



Chanzo: mwananchi.co.tz