Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashiru Ally awaonya ma- RC wanaosaka ubunge uchaguzi mkuu 2020

29649 Katibu+pic Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally

Mon, 3 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally ametoa onyo la mwisho kwa wakuu wa mikoa  nchini Tanzania kuacha kuvuruga chama hicho kwa kufanya kampeni kimyakimya ya kusaka majimbo huku wakitumia rasilimali za Serikali.

Dk Bashiru ametoa onyo hilo jana Ijumaa Novemba 30, 2018 wakati akizungumza na wanachama wa CCM Mkoa wa Geita katika ziara mkoani humo.

Amesema wakuu hao wa mikoa, wameshindwa kutumia nafasi zao kutekeleza majukumu waliyokabidhiwa na Rais John Magufuli na kubaki kujiimarisha wao jambo ambalo hataki kuliona likiendelea.

Amewataka wateule hao wa Rais  kufanya kazi ya heshima na ya kikatiba ya ukuu wa mkoa, badala ya kuanza kuvuruga chama katika maeneo mengine.

“Nitawapeleka kwa aliyewateua, nimwambie awatafutie kazi nyingine waache kuvuruga chama, kwa sababu katika hatua za kutafuta ubunge, wanasababisha chuki na fitina katika majimbo, waache hapakaliki, sasa waache kumdharau aliyewateua.”

“Huwezi kujenga uongozi wa pamoja kama wateule wa rais na viongozi wa kisiasa hawana mtazamo wa pamoja,” amesema Dk Bashiru.



Chanzo: mwananchi.co.tz