Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashiru Ally aongoza kikao hadi usiku

29853 Bashiru+pic Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally

Mon, 3 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Unaweza kusema kikao cha Halmashauri Kuu CCM Mkoa wa Geita kinachofanyika mjini hapa leo Jumapili Desemba 2, 2018 kimekumbwa na giza nene kutokana na kuanza saa 4 asubuhi, hadi kufikia saa 2:30 usiku kilikuwa bado hakijamalizika.

 

Kikao hicho kinachoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally kilianza kwa wajumbe kujitambulisha huku mmoja wao, Kassim Idd akiomba kuzungumza na kulalamika kitendo cha wajumbe kutopewa taarifa za ujenzi wa jengo la CCM la mkoa huo.

 

Kufuatia malalamiko ya mjumbe huyo, katibu mwenezi wa CCM, David Azaria aliomba wasiokuwa wajumbe wa kikao hicho kutoka nje ya ukumbi.

 

Azaria alipotafutwa baadaye na wanahabari kuzungumzia kikao hicho kutomalizika saa nane mchana kama ilivyopangwa amesema bado hawajafikia hata nusu ya ajenda kutokana na kuibuka mambo mbalimbali.

 

Amesema hawezi kuweka wazi kikao hicho kitamalizika muda gani na kuwataka wanahabari kusubiri hadi kitakapomalizika kwa ajili ya kupata taarifa wanazozihitaji.



Chanzo: mwananchi.co.tz