Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashe amtaka Ndugai agombee tena Ubunge

NDUGAI ED Spika wa Bunge, Job Ndugai

Tue, 12 Oct 2021 Chanzo: Mwananchi

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amemwomba Spika wa Bunge, Job Ndugai kubadili uamuzi wake wa kutogombea tena ubunge wa Kongwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Bashe ametoa kauli hiyo jana jioni Oktoba 11, 2021 wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa korosho wa wilaya za Mpwapwa, Kongwa na Manyoni.

Bashe amesema mipango mizuri ambayo imeanzishwa na Ndugai haipaswi kubezwa na kuwa akija mwingine huenda asiendeleze kwani kila mmoja ana mipango yake.

"Nilisoma kwenye mitandao kuwa ukitaka kustaafu na Rais John Magufuli, lakini Mungu ana mipango na makusudi yake, leo tuko na Samia Suluhu Hassan ambaye tunakwenda naye hadi 2030, naomba ufikiri namna ya kubadili uamuzi wako," amesema Bashe.

Chanzo: Mwananchi