Mon, 12 Mar 2018
Chanzo: bongo5.com
Mbunge wa Nzega Mjini kwa tiketi ya CCM, Mhe. Hussein Bashe amesema kuwa tayari ameshachukua hatua ya kuwasilisha hoja yake binafsi kwa Katibu wa Bunge na kudai kuwa ni wajibu wake kikatiba.
Bashe amesema kuwa hoja hiyo haijatoka hewani ameshafanya utafiti wa kutosha kwa zaidi ya miezi mitano juu ya matukio ya utekaji, mauaji na watu kupotea yaliyotokea tangu mwaka 2010.
Akielezea hoja hiyo mbele ya waandishi wa Habari leo Alhamisi Machi 08, 2018, Mhe. Bashe amesema ili chama chake kiendelee kuimarika ni lazima kisimamie misingi yake.
“Ili CCM iendelee kuimarika lazima isimamie misingi yake. Nakwenda bungeni na hoja hii kama mbunge wa CCM. Nimechukua hatua hii sababu ni kiapo changu kwa Chama Cha Mapinduzi. Siwezi kulalamika mitaani nitatumia nafasi yangu kuwasilisha jambo hili,” amesema Bashe.
Chanzo: bongo5.com