Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baraza la wazee la Chadema lasisitiza tume huru ya uchaguzi

65699 Pic+wazee

Sat, 6 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baraza la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  nchini Tanzania limesisitiza kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi katika chaguzi zote zijazo.

Mwenyekiti wa baraza hilo, Hashim Juma Issa amesema leo Ijumaa Julai 5, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuwa tume hiyo itasaidia kuwepo kwa uchaguzi huru wa watu kuchagua chama wanachotaka.

Kuhusu suala la aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kuvuliwa nafasi hiyo, Issa amesema kiongozi huyo ameonewa kwani licha ya kujeruhiwa kwa risasi vipo vielelezo vinavyoonyesha kuwa yupo kwenye matibabu.

Aidha baraza hilo limemuomba Rais wa Tanzania, John Magufuli kuandaa mkutano baina yake na viongozi wa vyama vya upinzani ili waweze kubadilishana mawazo.

"Ameshakutana na viongozi wa dini,  wafanyabiashara na makundi mengine hilo tunampongeza ndivyo utawala unavyotakiwa kuwa, lakini hajakutana na viongozi wa vyama vya siasa ili wapate nafasi kuzungumza naye," amesema mwenyekiti huyo wa baraza la wazee la Chadema.

Issa amesema katika utawala wao wanatarajia kuunda wizara ya wazee, baraza la taifa la wazee na kuwa na mbunge wa viti maalum mzee kwa ajili ya kuwakilisha kundi hilo bungeni.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz