Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Babu Duni Haji Mwenyekiti Mpya ACT Wazalendo

Babu Duni Haji.jpeg Babu Duni Haji

Sun, 30 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

#SIASA: Babu Juma Duni Haji ameshinda kiti cha Uenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho uliofanyika usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam, nafasi hiyo ilikuwa wazi baada ya kifo cha Maalim Seif Shariff Hamad.

Juma Duni Haji ameshinda kiti hicho baada ya kumshinda mpinzani wake Hamad Masud Hamad. Katika uchaguzi uliofanyika January 29 Juma Haji Duni akipata kura 339 dhidi ya 125 za mpinzani wake.

Juma Haji Duni anakuwa mwenyekiti wa tatu tangu kuasisiwa kwa chama hicho mwaka 2014.

Mwenyekiti wa kwanza ni hayati Anna Mghwira wa pili ni hayati Maalim Seif Sharif Hamad na sasa ni Juma Haji Duni.

Juma Haji Duni alikuwa mgombea mwenza wa mgombea wa chama Cha demokrasia na maendeleo CHADEMA ambae ni waziri mkuu wa zamani wa Tanzania mheshimiwa Edward Lowasa katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Tangu marekebisho ya katiba ya Zanzibar chama Cha ACT Wazalendo kimetoa makamu wa kwanza wa Rais mara mbili.

Othman Masoud Othman ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameshinda kiti cha Umakamu Mwenyekiti Zanzibar wa Chama cha hicho.

Aidha, kada wa chama hicho, Msafiri Mtemewa ameshinda nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live