Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba wa katibu wa Chadema aliyeuawa Singida amuachia Mungu yaliyotokea

97501 Pic+chadema+kifo Baba wa katibu wa Chadema aliyeuawa Singida amuachia Mungu yaliyotokea

Sat, 29 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Manyoni. Wakati mwili wa Alex Joas (40) aliyekuwa kiongozi wa Chadema wilayani Manyoni, ukitarajiwa kuzikwa leo, baba mzazi wa marehemu Joas Magubi amesema kifo cha mwanaye kimemuachia maswali matatu, lakini anamwachia Mungu.

Alex atazikwa mchana leo Jumamosi Februari 29, 2020 katika makaburi ya Kaloleni mjini Manyoni baada ya kukamilika kwa taratibu za maandalizi.

Mwili wa Alex ulikutwa pembeni mwa njia ukiwa na majeraha makubwa matatu usoni hali inayoonyesha alikatwa na kitu chenye ncha kali hata kusababisha meno ya juu upande wa kushoto kung'ooka.

Mzee Magubi amesema bado anashangazwa kuona mtoto wake akiuawa kikatili lakini wauaji wakaacha pikipiki, hawakuchukua fedha lakini akahoji mboja waliondoka na simu ambayo ingesaidia upelelezi. "Nilifika hospitali kushuhudia mwanangu alivyokatwa zaidi ya mnyama mkorofi, pikipiki waliacha tena imesimama, funguo za pikipiki wakaweka kwenye mfuko wa shati, hawakuchukua kitu hivi kweli ni mauajia ya ujambazi haya? Anahoji Magubi.

Kwa mujibu wa mzee huyo, hajawahi kusikia kama mtoto wake huyo alikuwa na kisa na mtu mwingine na kuwa alikuwa ni mtu wa kujichanganya na watu wote na ilikuwa nguzo katika familia. Amesema huyo ni mtoto wake wanne kati ya watoto 7 na kuwa anaumia zaidi anapowaona watoto wa marehemu wawili aliowaacha hivyo mashitaka yake mtoa hukumu ni Mungu.

Jana mafundi walikamilisha ujenzi wa kaburi la kiongozi huyo licha ya changamoto ya mvua iliyokuwa ikinyesha na majira ya usiku nyumbani kwa marehemu mtaa wa Majengo kulikuwa na watu wachache kutokana na mvua huku bendera za Chadema zikitawala kila kona.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz