Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BREAKING: Sugu ameachiwa kwa dhamana

Video Archive
Mon, 12 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Emmanuel Masonga wanaokabiliwa na kesi ya kutoa lugha ya fedheha kwa Rais Magufuli wameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu mkazi Mbeya.

Baada ya upande wa washtakiwa kumaliza kutoa ushahidi wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala, Sugu na Masonga wamejidhamini wenyewe kwa dhamana ya Milioni 5. Hukumu ya kesi hiyo itatolewa February 26, 2018.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite amewaachia kwa dhamana wote wawili baada ya Wakili upande wa utetezi, Peter Kibatala kuiambia Mahakama ameshafunga ushahidi wake ambapo mashahidi sita walitoa ushahidi wao.

Mawakili wa pande zote mbili walikubaliana kwamba February 19, 2018 watawasilisha majumuisho ya shauri hilo Mahakamani hapo.

Hakimu Mteite amekubaliana na hoja hiyo ya Mawakili na kusema hukumu ya kesi hiyo itatolewa February 26, 2018  “Washtakiwa wote wanaachiwa kwa dhamana na kila mmoja atajidhamini mwenyewe kwa hati ya dhamana ya maneno ya shilingi Milioni 5 kila mmoja .

Mbunge Joseph Mbilinyi na Katibu Emmanuel Masonga walishikiliwa na Polisi tangu January 2, 2018.

ALICHOZUNGUMZA DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA KESI YAKE NA HAMISA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Chanzo: millardayo.com