Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BREAKING: Makada 19 wa Chadema waachiwa huru

Makada Chadema Huru Makada 19 wa Chadema waachiwa huru Mwanza

Wed, 1 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi na wanachama 19 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walioshtakiwa kwa madai ya kufanya fujo wakati wa ibada katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kawekamo jijini Mwanza wameachiwa huru.

Wana Chadema hao wameachiwa huru leo Jumatano Juni Mosi, 2022 na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo namba 77/2021.

Kwa mara ya kwanza, wanachama hao walifikishwa mahakamani Agosti 19, 2021 wakidaiwa kutenda kosa hilo Agosti 15, 2021.

Washtakiwa kwa pamoja walidaiwa kuhudhuria Misa ya Jumapili katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kawekamo wakiwa wamevaa sare za chama chao na fulana nyekundu zilizoandikwa Katiba Mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live