Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BAWACHA walaani unyanyasaji wa Polisi

BAWACHA2 Baraza la Wanawake Chadema

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Wanawake CHADEMA, BAWACHA, limesikitishwa na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa wanawake wa Chama hicho unaofanywa na jeshi la Polisi katika Mahabusu mbali mbali za jiji la Dar es Salaam kwa kuzuia wasipewe taulo za kike na kuonana na mawakili pamoja ndugu zao.

Baraza hili limeelezwa kuwa lina laani vitendo hivyo ambavyo vinawadhalilisha wanawake hao huku likiendelea kuwashikilia pasipo kuwapeleka Mahakamani

Wamesema kuwa hawatakaa kimya wala kurudi nyuma katika kupinga uonevu huo unaofanywa chini ya serikali ya Rais Samia ambaye yupo kimya huku nwananchi wake wakibambikiziwa kesi za ugaidi na wanawake wakidhalilishwa Mahabusu.

Viongozi hao wa Bawacha walikamatwa katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu walipofika kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wao Freeman Mbowe anaekabiliwa nakesi ya Ugaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live