Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BAWACHA Arusha wampigia magoti Rais Samia

Bawacha Pic Data BAWACHA wampigia magoti Rais Smia

Fri, 10 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Baraza la Wazee Chadema (Bawacha) Jimbo la Arusha mjini wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kukaa pamoja katika ili kujadili mustakabali wa kuondoa tofauti zao za vyama vya kiasa na kuwa kitu kimoja.

Akizungumza na waandishi wa habari Desemba 9, 2021 Mwenyekiti wa Bawacha Jimbo la Arusha mjini,Emmanuel Zakaria amesema wanaomba maridhiano ya kitaifa ili haki itendeke kwa lengo la kuleta umoja wa vyama vya siasa nchini.

"Njia ya kuleta umoja ni kukaa meza moja katika kujadiliana kwa lengo la kupata muhafaka wa maridhiano kama ilivyo Zanzibar kwani hatuwezi tukafika hivyo inabidi tuige mfano wa Rais mstaafu Aman Abed Karume nakupata ujasiri aliyoutumia kuleta suluhu Tanzania visiwani,"amesema Mwenyekiti huyo.

Zakaria amesema sasa hivi Tanzania visiwani ipo amani katika vyama vya siasa kutokana na maridhiano yakukaa pamoja lakini kwa upande wa bara wamechoshwa na siasa za upande mmoja hivyo ni vyema wakakutana na Rais Samia kwa lengo la kuleta umoja na maendeleo nchini.

Mwenyekiti huyo amesema Rais Samia hana shida yeyote isipokuwa washauri kwani alipoingia madarakani alianza vizuri hadi wapinzani tulimuunga mkono hali iliyopelekea kukosa hoja kwa upande wao lakini wanashangaa kubadilika.

"Tunaomba Rais Samia arejee hotuba yake ya bungeni kwani sisi wazee wa Jiji la  Arusha tunaunga mkono maombi ya balozi wa Marekani aliyesema anatamani bara kuwe na maridhiano kama Zanzibar kwani najua hii ndio njia ya kuliponya Taifa hili,"amesema Zakaria.

Advertisement Hata hivyo amemuomba Rais Samia katika hotuba zake ajikite  katika changamoto za wananchi wake kwani kuna mifumuko ya bei ya vitu mbalimbali hali ambayo wenye maisha ya chini wanashindwa kukidhi.

Aidha amesema ni vyema wangewekeza zaidi katika rasilimali watu kwa kuanzia shuleni,wanafunzi wakapata chakula ambacho kinajumuisha mlo kamili ili kupata Taifa lenye nguvu katika kizazi cha sasa na kijacho.

Amesema kwa kufanya hivyo kutasaidia kupata Taifa lenye nguvu,wabunifu,hodari katika matumizi ya teknolojia pamoja na michezo.

Grace Liazer ambaye ni mjumbe wa baraza hilo amesema wanamuomba Rais Samia ajikite pia katika masuala ya bima kwa wananchi wote kwani wengi wao wanashindwa kumudu gharama za matibabu.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz