Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BAVICHA wataka Jeshi la Polisi lisimamiwe

BAvichaaaaaaaaaa BAVICHA wataka Jeshi la Polisi lisimamiwe

Mon, 11 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) limependekeza kuanzishwa kwa chombo huru kitakachosimamia utendaji wa Jeshi la Polisi, ili kuepuka malalamiko yanayotolewa na wananchi.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Julai 11, 2022 Mratibu wa Uhamasishaji Bavicha, Twaha Mwaipaya ikiwa ni wiki moja tangu alipoachiwa kwa dhamana jijini Dodoma.

Juni 30 Mwaipaya alikamatwa na Jeshi la Polisi akiwa akiwa eneo la Tarminal Pub Msamvu nakusafirishwa kwenda Dodoma kisha Dar es Salaam, kalba ya kurudishwa Dodoma ambapo Julai 6 aliachiwa kwa dhamana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini hapa, amesema baada ya kukamatwa na Jeshi la Polisi alizungushwa vituo mbalimbali, huku akinyimwa haki zake za msingi ikiwemo kuwasiliana na mwanansheria wake na ndugu.

"Nilikamatwa Juni 30 wakati nipoenda kula na wenzangu wa Bavicha Mkoa wa Morogoro, na kupelekwa kituo kikuu cha polisi,"amesema Mwaipaya.

"Tangu nakamatwa hadi nafikishwa kulituo cha Polisi wakikuwa wakinitaka niwape simu bila kuniambia kosa langu, ambayo hata hivyo waliichukua,"alisema Mwaipaya.

Advertisement Akizungumzia hali aliyokutana nayo kwenye vituo vya Polisi Mwaipaya amesema, ni pamoja na watuhumiwa kushikiliwa kwa kwa zaidi ya wiki tatu, kinyume na sheria.

Alipoulizwa na Mwananchi kuhusu madai ya Mwaipaya, Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime amesema kesi zilizopo kituoni hazifanani, hivyo kama Kuna mtu anashikiliwa kwa muda mrefu inategemea na aina ya kesi.

"Kama yapo majina ya watu walioshikiliwa kwa kipindi chote hicho, waweke walete majina ili niweze kufuatilia na kutoa taarifa ya Polisi," amesema Misime.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live