Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BAVICHA walaani Mbowe kushambuliwa

BAVICHA.webp BAVICHA walaani Mbowe kushambuliwa

Fri, 12 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Vijana la Chadema, Bavicha wilayani Shinyanga, limelaani tukio la Mwenyekiti wa Chadema hicho Taifa, Freeman Mbowe, kushambuliwa na watu wasiojulikana akiwa Jijini Dodoma na kuvunjika mguu.

Hayo yamebainishwa leo Juni 12, 2020 na Mwenyekiti wa Baraza katika wilaya hiyo, Samson Ngw’agi wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuendelea kutokea kwa matukio ya kushambuliwa viongozi wakubwa wa chama hicho.

Amesema tukio la kushambuliwa kwa Mbowe linapaswa kupingwa na kila mtu likiwamo na tukio la Tundu Lisu, na kueleza vitendo hivyo vina ashiria ukosefu wa amani hapa nchini, kutokana na kuendelea kwa matukio hayo huku wahusika kutokamatwa.

“Sisi Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Bavicha Wilaya ya Shinyanga mjini, tunalaani tukio la kushambuliwa kwa Mwenyekiti wetu wa Taifa Freeman Mbowe Juni 9 Mwaka huu akiwa Jijini Dodoma na watu wasiojulikana,” amesema Ng’wagi.

“Tunaomba Jeshi la Polisi lifanye uchuguzi wa kina juu ya tukio hilo bila upendeleo, pamoja na kukitafuta kikundi cha watu wasiojulikana, lihakikishe linakitafuta sababu kimekuwa tishio kwa viongozi wetu wakubwa kwa kuwashambulia akiwamo na Tundu Lisu lakini hawakamatwi,” amesema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live