Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Gwajima awasili Dodoma, kuhojiwa na Kamati ya Maadili

Bungeni Gwajima Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe

Mon, 23 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tayari Mbunge wa Jimbo la Kawe, Josephata Gwajima amewasili ndani ya viunga vya Bunge la Tanzania kwa ajili ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili leo jijini Dodoma.

Mbunge huyo alipokea wito huo mara baada ya kuwepo kwa vuta ni kuvute baina yake na Waziri wa Afya, Dorothy Gwajima juu ya chanjo ya UVIKO-19.

Hata hivyo Mbunge huyo alithibitisha kupokea wito huo, huku akilaani kitendo cha barua ya wito kuanikwa katika mitandao ya kijamii, mbali na hayo alisisitiza kuwa atafika katika kamati hiyo hii leo.

Wito huo pia umemtaka Mbunge wa Ukonga, Jerry Slaa, kufika mbele ya Kamati hiyo kwa ajili ya mahojiano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live