Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Gwajima awasha moto tena Bungeni

Gwajima Hj Askofu gwajima

Fri, 27 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Jimbo la Kawe kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mchungaji Josephat Gwajima amesema migogoro ya ardhi Wilaya ya Kinondoni inachochewa na Viongozi wa Serikali.

Gwajima amesema Wilaya ya Kinondoni ndiyo kinara wa migogoro ya ardhi na viongozi wa Serikali badala ya kutatua migogoro ya ardhi lakini inawachonganisha wananchi na kuwagombanisha na Serikali yao.

Mbunge Gwajima ametolea mfano tukio la kubomolewa kwa nyumba 103 katika eneo la Mbweni mpiji ambapo anadai matrekta na matingatinga yalibomoa nyumba hizo bila amri ya Mahakama au Mamlaka yoyote ile ya Kiserikali.

Muwakilishi huyo wa jimbo la Kawe ametamka maneno hayo wakati akichangia hoja kwenye Bunge la Bajeti, Mkutano wa 7 Kikao cha 32 ambapo Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inawasilisha Makadirio ya Bajeti yake ya Mwaka wa Fedha 2022/2023.

Gwajima alibainisha kuwa baada ya kufuatilia aliambiwa kuwa lile ni eneo maalum kwa ajaili ya kujenga bustani ya Wizara na kushangazwa na tukio la kubomolewa kwa nyumba za wapiga kura huku Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni naye akisema kuwa hakutoa maelekezo yoyote juu ya kubomolewa kwa nyumba hizo.

Kwa upande mwingine Mchungaji Gwajima ametoa pongezi kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete pamoja na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye kwa ushirikiano wao kwa kutumia masaa mawili kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 30 katika eneo la Mtaa wa Jogoo na Ndumbwi Jimbo la Kawe ambako kuna nyumba zaidi ya 4500.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live