Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Gwajima: "Niko tayari kupoteza Ubunge lakini chanjo HAPANA"

97978 Gwajima+pic Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima na Mbunge wa jimbo la Kawe Josephat Gwajima

Mon, 16 Aug 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima na Mbunge wa jimbo la Kawe Josephat Gwajima ameendelea na msimamo wake wa yeye na waumini wake kutochanjwa, akieleza kuwa Bunge likilazimisha hatochanjwa.

Hata hivyo, ufafanuzi uliotolewa na Ofisi ya Bunge hivi karibuni umesema hakuna mbunge aliyelazimishwa kupata chanjo hiyo.

Akizungumza katika ibada yake Agosti 15, Gwajima amesema chanjo hiyo inayoendelea kutolewa nchini hazijafanyiwa utafiti wa kina kubaini madhara yake kwa wanaochanjwa na vizazi vijavyo.

“Wanaotaka nifukuzwe CCM watumie akili, kwa mfano tukichanja wote halafu kufikia 2025 watu wako hoi tunapigaje kampeni, bora wengine tubaki tusaidie kutetea chama chetu,”.

“Kulikuwa na twitter inasambaa kwamba wabunge wote wachanjwe, baadae Ofisi ya Bunge ikakanusha nikasema hata ingekuwa kweli mie nisingechanjwa, ni heri kurudi hapa nyumbani, ubunge ni mzuri una heshima unasaidia wananchi lakini kunichanja hapana,” amesema askofu Gwajima.

Hata hivyo amesema hapingi chanjo kwa ujumla wake: “Sipingi chanjo ila hii haijafanyiwa tafiti za kutosha kwa maana hiyo nasema hapa hachanjwi mtu. Mimi sio adui yenu nalinda kizazi chenu kijacho na Tanzania yetu ijayo kwa nguvu zangu zote.”

Chanzo: www.mwananchi.co.tz