Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Bagonza ataka mazungumzo ya katiba mpya yaanze

Bagonzaa Askofu Bagonza ataka mazungumzo ya katiba mpya yaanze

Tue, 8 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Askofu wa Dayosisi ya Karagwe ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Benson Bagonza ameshauri kuwepo kwa mazungumzo mema kwa ajili ya upatiikanaji wa katiba mpya kabla hali haijabadilika kuwa mbaya.

Askofu Bagonza ametoa kauli hiyo leo Machi 8, 2022 wakati anahutubia kongamano la Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) lililofanyika mkoani Iringa, ikiwa ni kusherekea siku ya wanawake duniani.

Katika maelezo yake amewataka wananchi kutambua kuwa vyama vyote vilivyopo nchini ni vya viongozi kabla havijawa vya wanachama, hivyo ni imani yake kwamba vyama hivyo vitaanza mazungumzo kushughulikia suala la katiba kutokana na umuhimu wake.

“Yako mambo yanayohitaji maridhiano, kwa mfano katiba mpya tuanzie wapi na tuanze lini, tuanze na vipengele vipi chonganishi na vipi ninavyoona mimi katiba ilihitajika toka jana kuliko leo.  Tumechelewa kwa sababu hatujakubaliana tuanzie wapi mazungumzo yenye nia njema yaanze kwanza kabla hali haijabadilika kuwa mbaya,” amesema Askofu Bagonza

Hata hivyo, amesema hata kama katiba mpya ikipatikana, haitajibu kila tatizo nchini, kwani utamaduni wa kutojali katiba una nguvu kuliko katiba yenyewe.

“Mazoea ya kutoheshimu katiba yana nguvu kuliko katiba yenyewe. Wanaovunja katiba mbovu tuliyonayo ndiyo hao watakao vunja katiba mpya, lakini kibinadamu ni vema kuwa na katiba nzuri inayovunjwa na watawala wabaya kuliko kuwa na katiba mbaya na watawala mbaya,” ameseMA

Aidha, Bagonza amesema hakuna umilele wa chama chochote kilichoundwa na mwanadamu kitakachotawa taifa milele huku akieleza watu wanaalikwa kupokea mabadiliko wasiyopenda katika maisha yao.

“Sheria kandamizi hutengenezwa na watu wenye dhuluma na ukandamizaji na ni matokeo ya watu wenye fikra za dhuluma. Zisipofutwa zina tabia ya kuwatafuna waliozitunga. Siku zote tunaalikwa kutenda haki katika kutunga sheria kwa sababu hatuna mamlaka juu ya kesho yetu,” amesema.

Bagonza: Siku ya wanawake ni kupambana na ukandamizaji

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dk Benson Bagonza amesema Siku ya Wanawake Duniani ni tunda la harakati dhidi ya mifumo iliyokuwa ikiwakandamiza. Soma zaidi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live