Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

...Asema Chadema itashinda Monduli

14615 MONDULI++PIC TanzaniaWeb

Thu, 30 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mto wa Mbu. Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema Chadema ipo imara na itashinda Jimbo la Monduli.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za Jimbo la Monduli zilizofanyika Kata ya Mto wa Mbu jana, Lowassa aliwataka wananchi kupuuza propaganda kuwa Chadema itakufa.

Lowassa alisema hayo huku akiyataja maendeleo aliyoleta Monduli katika kipindi chake cha ubunge zaidi ya miaka 20.

Alisema aliingia ubunge Monduli kukiwa na shida ya maji, barabara, umeme na ardhi, lakini alishughulikia na sasa kila Mtanzania anajua.

Alisema kumekuwepo na maneno kuwa amerejea Monduli kulinda ngome ya Chadema jambo ambalo sio sahihi. “Chadema bado tupo imara na tutashinda.”

Lowassa alieleza kuunga mkono, tamko la Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kuzuia polisi kutekeleza maagizo ya wakuu wa wilaya na mikoa kukamata watu bila sababu za msingi.

Alisema kumekuwepo na matukio ya kukamatwa watu bila sababu za msingi, hivyo uamuzi wa waziri unapaswa kupongezwa.

Lowassa aliwataka wakazi wa Monduli, kumchagua mgombea na Chadema, Yonas Laiser kwani ndiye atawaletea maendeleo.

Kwa upande wake, Laiser aliomba wananchi kumchagua kwani anajua kero zao na atashirikiana na Lowassa na madiwani kuzitatua.

Laiser alisema amekuwa akifuatwa kutakiwa kujiuzulu kugombea ubunge na udiwani na atapewa cheo serikalini lakini amegoma. “Kwa muda mrefu wananifuata niwasaliti wananchi, mimi nimesema hapana, sihami Chadema na sina chama kingine zaidi ya Chadema,” alisema.

Meneja wa kampeni, Patrick ole Sosopi aliwataka wakazi wa Monduli kujitokeza kupiga kura na wapuuze propaganda kuwa hata kama mgombea wa Chadema akishinda hatatangazwa.

Sosopi pia alionya njama zozote za kuiba kura ama kuhujumiwa katika uchaguzi huo kwamba Chadema haitakubali.

Chanzo: mwananchi.co.tz