Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Angeline Mabula ampongeza Jerry Silaa, amuahidi ushirikiano

Mabula 783.png Angeline Mabula ampongeza Jerry Silaa, amuahidi ushirikiano

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Ilemela, ambaye alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula amesema ametua kijiti kwa Jerry Silaa na kumuahidi ushirikiano.

Dk Mabula ambaye ni miongoni mwa mawaziri waliopumzishwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, wiki iliyopita, amesema hayo bungeni mjini Dodoma aliposimama kwa ajili ya kuuliza swali la nyongeza kwenye Wizara ya Maji na kueleza kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano kwa mrithi wake katika wizara hiyo.

Katika swali lake la nyongeza, Mbunge huyo aliulizia kuhusu mradi wa chanzo kipya cha maji Jimbo la Ilemela, ambapo akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi, amesema wataalamu wanaendelea na kazi waliyopewa na kwamba katika mwaka huu wa fedha jambo hilo litafanyiwa kazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live