Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi amesema mtu yeyote anayetaka maradaka kwa mafarakano hafai ndani ya CCM.
"Mtu yeyote anayetafuta madaraka kwa mafarakano, kwa misingi ya ukabila, kwa misingi ya dini hawafai kuwa kiongozi wa serikali wala katika chama chetu cha mapinduzi, kila mtanzania anatakiwa kukumbuka kuwa viongozi sahihi wataisimamia serikali sahii"
"Chama kibovu kitazaa serikali mbovu, chama kisicho makini kitazaa serikali isiyo makini, chama imara kinaanza kujengwa katika mashina, tutambue kwamba hiyo ndio ngazi ya kwanza ya umuhimu wa pekee katika chama chetu na wao watambue wao ndio wa kwanza kuusimamia wajibu wa wananchama"
"Hii ndicho chama pekee kinachoongelea majukumu ya chama kwa wanachama wake na huwezi kuyatenganisha mafanikio ya serikali na CCM kwakuwa CCM madhubuti ndio yenye kuleta maendeleo kwa taifa hili."
Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi Katibu Mkuu wa CCM