Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anayejiamini mkubwa kuliko CCM ajitokeze

49a66d794522c167ec90166638667294 Anayejiamini mkubwa kuliko CCM ajitokeze

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

“Kama kuna mtu anaamini yeye ni mkubwa kuliko CCM aseme hadharani, ili chama kiweze kuchukua hatua lakini sio unakaa sehemu unajifungia unamtweza Rais wetu, halafu sisi vijana wa CCM tukae kimya, hiyo dhambi hatutakubali kuifanya hata siku moja,”Katibu Mkuu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kenan Kihongosi akizungumza leo mkoani Iringa na kuongeza

“Sisi UVCCM hatutavumilia mtu anayemvunjia heshima ya Rais wetu, tutasimama, tutamlinda Rais wetu na tunasema wazi kabisa, yeyote anayetaka kumkwamisha Rais wetu atakwama yeye kabla hajamfikia na huo ndiyo msimamo wetu kama UVCCM,” amesisitiza

Kenani ametoa kauli hiyo leo na kudai kuwa UVCCM inahoji kwa nini makelele juu ya Serikali kukopa fedha za utekelezaji miradi ya maendeleo, yaibuke baada ya Rais Samian Suluhu, kuingia madarakani.

Katibu Mkuu huyo wa UVCCM amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia, sio ya kwanza kukopa, kwani hata awamu zilizopita zilikopa.

“Kumekuwa na matamko yasiyoeleweka, baadhi ya viongozi ambao tunawaheshimu katika Serikali hii, wameenda mbali wanakosoa na kuona mikopo hii haina tija. Sasa niseme, tangu Awamu ya Kwanza kwa Mwalimu Julius Nyerere na leo ya Rais Samia, hakuna awamu haikukopa fedha, kwa nini haya makelele yaanze baada ya Awamu ya Sita kuwa madarakani?” Amesema Kihongosi.

Mwanasiasa huyo amesema kuwa, hakuna nchi na au mtu asiyekopa na kwamba hata wabunge bungeni wana mikopo mikubwa.

“Kubwa zaidi, duniani kote hakuna nchi ambayo haikopi fedha, hata ninyi kwenye familia zenu mnadaiwa. Watu mmekopa mabenki huko, mmeweka amana mbalimbali. Wabunge ndani ya Bunge wamechukua mikopo mikubwa, hili jambo linajulikana nani ambaye hakopi?” Amesema Kihongosi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz