Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ally Hapi: Kinana ana mkubwa

Kinana Ally Hapi Ally Hapi: Kinana ana mkubwa

Fri, 1 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi amesema kuwa Abdulrahman Kinana ambaye jina lake limependelezwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni mtu mwenye uwezo mkubwa na kuwataka wanaCCM kuachana na mambo ya nyuma.

Kauli yake hii inakuja kutokanana na swali aliloulizwa na wanahabari nje ya ya ukumbi wa Jakaya kikwete unakofanyika mkutano mkuu wa CCM jijini dodoma ambapo amesema kuwa mambo yaliyopita hayana msingi kwa sasa.

"Hakuna ubishi juu ya uwezo wa Mzee Kinana" ameeleza Hapi

Hapi ameeleza kuwa Kinana ni mtu mwenye uwezo, maarifa na uzoefu mkubwa kwenye siasa na ni mwalimu kwa watu wengi kwenye chama hicho.

"Kama vijana ambao tunaendelea kujifunza kwenye siasa za chama mambo ya nyuma nadhani hayana msingi kwa sasa hivi" aliongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live