Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyekuwa makamu mwenyekiti NCCR-Mageuzi atangaza kurejea CCM

11365 Nncr+pic TanzaniaWeb

Sat, 14 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti NCCR-Mageuzi (Bara), Leticia Mosore leo Ijumaa Julai 13, 2018 ametangaza kurejea CCM.

Akizungumza na waandishi wa habari Mosore amesema aliamua kuhama CCM kwa kuwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho haukuwa wa kuridhisha.

Akiwa na wanachama wengine watano wa NCCR waliohamia CCM, Mosore ametaja sababu nyingine kuwa ni rushwa na ukosefu wa maadili, akidai kuwa zilikuwa hoja kuu za upinzani lakini kwa sasa zinatekelezwa ipasavyo na Serikali ya Awamu ya Tano.

“Kipindi cha uongozi wa Rais John Magufuli kwa miaka hii miwili ameshughulikia kweli kweli suala la rushwa na maadili. Serikali inafanya kazi kwa uwazi, ukusanyaji wa mapato ni mzuri. Pia imedhibiti matumizi yasiyo ya lazima,” amesema.

Wengine waliotangaza kujiunga na CCM ni aliyekuwa mjumbe wa halmashauri kuu  ya NCCR, Mchata  Mchata; aliyekuwa Katibu Jimbo la Segerea,  Lilian Kitunga; aliyekuwa  Katibu wa wanawake Segerea, Nossy  Chacha pamoja na Vedalin Nicholaus  na Eunice Zarcharia.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz