Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyekuwa DC abwagwa uchaguzi CCM Geita

CCM WEB Aliyekuwa DC abwagwa uchaguzi CCM Geita

Mon, 26 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita mwaka, Herman Kapufi ameshindwa kung’ara katika uenyekiti wa umuiya ya Wazazi ya CCM baada ya kuambulia kura 82 kati ya kura 801 zilizopigwa jana Septemba 25 wilayani hapo.

Kapufi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya mwaka 2016 hadi 2018, alikuwa miongoni mwa wagombea watatu nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Nyankumbu iliyopo mjini Geita.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo usiku wa kuamkia leo Septemba 26 majira ya saa sita usiku msimamizi wa uchaguzi, John Izack amemtangaza Robert Mwamaigolo kuwa mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo Wilaya ya Geita kwa kupata kura 694.

Herman Kapufi alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 82 na Kija Lusulukali alipata kura 23, huku kura mbili zikiharibika.

Akishukuru baada ya kupata ushindi huo, Mwamaigolo amesema atasimamia misingi ya chama kwa kujenga umoja pamoja na kuhakikisha jumuiya ya wazazi inapata maendeleo kupitia miradi mbalimbali iliyopo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live