Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyejitoa ACT Wazalendo sasa katibu mkuu mpya CUF

Aliyejitoapic Data Hamad Masoud Hamad

Mon, 28 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Wananchi (CUF) kimemteua Hamad Masoud Hamad kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, akichukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Haroub Mohamed Shamis.

Masoud ameteuliwa kushika wadhifa huo, akitokea Chama cha ACT Wazalendo alikokuwa akilalamika kuchezewa rafu katika uchaguzi aliogombea nafasi ya Mwenyekiti, ambapo Juma Haji Duni ndiye aliyechaguliwa kushika nafasi hiyo.

Baraza hilo pia limewateua Kona Vuai Haji na Juma Shaaban Nkumbi kuwa wajumbe wa baraza kuu huku nafasi nyingine zilizo wazi zikipangwa kujazwa katika kikao kijacho cha baraza kuu.

Kauli hiyo imetolewa leo Machi 28 jijini hapa na Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba wakati wa kutangaza maazimio ya ajenda 14 zilizotokana na mkutano wa baraza hilo, ikiwamo mabadiliko ya uongozi, hali ya ngumu ya maisha, vita vya Urusi na Ukraine na hali ya kisiasa.

“Baraza Kuu limemshukuru Haroub Mohamed Shamis kwa kazi kubwa aliyofanya kama Katibu Mkuu katika kipindi kigumu baada ya kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama, hayati Khalifa Suleiman Khalifa na kukiwezesha chama hicho kushiriki kikamilifu katika uchaguzi Mkuu wa 2020,” amesema Lipumba.

Azimio lingine la baraza hilo ni pampoja na kuweka kando masharti ya Ibara ya 116 kifungu kidogo cha 6 yaliyopo kwenye Katiba ya chama hicho ya mwaka 1992 Toleo la 2019, yanayozuia mwanachama mpya kugombea nafasi ya uongozi hadi atakapokuwa ametimiza miezi sita.

Advertisement Baraza hilo pia limeondoa kikwazo hicho ili kuhakikisha wanachama wanaorejea ndani ya chama hicho kushiriki katika ujenzi wa chama hicho huku likitangaza kuanza kwa uchaguzi wa ndani kati ya Mei 14 mwaka huu hadi Oktoba 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live