Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichosema Makonda alipozuru kaburi la Mkapa

Makonda Mkapa Kaburi (600 X 313) Alichosema Makonda alipozuru kaburi la Mkapa

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda ametembelea kaburi la aliyekuwa Rais wa awamu ya 3, hayati Benjamin William Mkapa katika Kijiji cha Lupaso mkoani Mtwara.

Makonda ametembelea kaburi hilo leo Februari 12, 2024 na kutoa pole kwa familia, huku akiongeza kuwa pole huwa haina mwisho kwa kuwa hakuna familia inayobaki na furaha baba anapoondoka.

Kiongozi huyo ametembelea kaburi hilo akiwa njiani kurejea jijini Dar es Salaam baada ya kukatisha ziara yake mkoani Ruvuma ili kupisha mazishi ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

View this post on Instagram

A post shared by Mwananchi (@mwananchi_official)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live