Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichosema Magufuli baada ya kuchukua fomu Urais

JPMA Alichosema Magufuli baada ya kuchukua fomu Urais

Wed, 17 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa CCM Dkt Magufuli leo Juni 17, 2020 amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Magufuli amechukua fomu kupitia chama chake cha CCM. Fomu hiyo amekabidhiwa na Katibu Mkuu Dkt Bashiru Ally asubuhi hii jijiji Dodoma.

Baada ya kukabidhiwa, Dkt Magufuli amezikagua fomu na kuahidi kutafuta wadhamini ndani ya siku 13 ili aweze kurejesha fomu hiyo ili kuendana na matakwa ya kanuni za chama hicho.

''Asante sana Katibu Mkuu, naomba nianze hili zoezi la kutafuta wadhamini kwa Mwenyekiti wa CCM hapa Dodoma naye anidhamini na nitaenda mikoa yote kwasababu nimekuwa nikipigiwa simu wanataka kunidhamini hivyo naamini nitarejesha fomu yangu kwa wakati'', amesema.

Aidha Dkt Magufuli amesema amechukua fomu hiyo kwaajili ya kuomba nafasi ya kuipeperusha bendara ya CCM pamoja na Ilani nzuri ambayo imeandaliwa kwaajili ya miaka mitano ijayo.

Kwa mujibu wa muongozo uliotolewa na Katibu mwenezi wa CCM Taifa Ndugu Humphrey Polepole mwisho wa kurejesha fomu ni Juni 30, 2020.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live