Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichokisema mbunge CCM siku moja kabla ya kifo chake

92032 Pic+mbunge Alichokisema mbunge CCM siku moja kabla ya kifo chake

Thu, 16 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Newala. Waziri wa Maji nchini Tanzania, Profesa Makame Mbarawa amesema amefika Newala kwa mwaliko wa aliyekuwa mbunge wa Newala vijijini (CCM), Rashid Akbar na kwamba waliwasiliana siku moja kabla ya kifo chake.

Mbunge Akbar alifariki jana Jumatano Januari 15,2020 Mingoyo mkoani Lindi na atazikwa leo Alhamisi katika kijiji cha Chihangu wilayani Newala.

Profesa Mbarawa ambaye yuko mkoani Mtwara toka jana asubuhi Jumatano akizungumza wakati wa utoaji salamu za rambirambi amesema wakati wa ratiba ya ziara yake mkoani Mtwara marehemu Akbar alimuomba kufika katika jimbo lake ili kuona namna ya kuendelea kutafuta changamoto za maji zinazowakabili wananchi.

“Marehemu amenialika mara nyingi na hata juzi nilipowasiliana naye kuhusu safari yangu hii (ziara) marehemu amekuwa mtetezi mkubwa wa wananchi wake tangu nikiwa wizara ya mawasiliano aliandika sana kuhusu mambo ya mawasiliano lakini pia amekuwa akisukuma sana changamoto za maji katika jimbo lake,” amesema Mbarawa

Amesema katika jimbo la Newala vijijini lililokuwa likiongozwa na mbunge huyo lina changamoto kubwa lakini walikuwa wakifanya kazi kwa karibu kuhakikisha wanaondokana na changamoto hiyo na baadhi ya maeneo walianza kupata maji.

“Katika mipango yetu tuliyokuwa tumepanga juzi tupitie maeneo mbalimbali tuhakikishe kule kwenye changamoto za miradi ya maji tunazimaliza lakini mwenyezi Mungu anayajua tusioyajua amemuondoa ndugu yetu na sisi tulimpenda lakini Mwenyezi Mungu amefanya ya kwake kazi kubwa tuliyokuwa nayo ni kumuombea kwa Mwezi Mungu amuweke mahala pema peponi,” amesema Profesa Mbarawa

Aidha amewataka wafiwa kuwa na moyo wa subra katika kipindi kigumu walichokuwa Nacho na kumtegemea Mwenyezi Mungu.

Profesa Mbarawa yuko mkoani Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi katika wilaya ya Mtwara,Newala na Masasi.

Chanzo: mwananchi.co.tz