Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichokisema January Makamba kuhusu tatizo la umeme jimboni kwake

Bumbuli Mbunge jimbo la Bumbuli January Makamba.

Tue, 3 Aug 2021 Chanzo: fullshangwe

Mbunge Jimbo la Bumbuli Mkoani Tanga January Makamba amesema kata tatu ambazo hazina umeme kabisa za Milingano ,Kwemkomole na Kisiwaniatahakikisha vijiji na vitongoji vya halmashauri hiyo ambavyo havijafikiwa na umeme vinafikiwa ili viweze kuondokana na changamoto ya giza .

Mbunge huyo alisema kuwa alipoingia madarakani aliahidi kupeleka umeme kila Kijiji na ahadi hiyo ameitimiza kwa kiasi kikubwa na Sasa anapigania kata zilizobaki zinapate ili awamu nyingine aanze na vitongoji vyote katika Jimbo la bumbuli.

” Kama umeme huu ungekuwa haujafika kabisa arafu Mbunge akaahidi kupeleka kwenye vitongoji basi ujue huyo ni tapeli naomba muendelee kusubiri umeme utafika kwani maendeleo yakipatikana ata Mimi mbunge nafurahi”Alisema Makamba.

Alisema kuwa dalili yakwamba umeme utafika maeneo yote tayari baadhi ya nguzo zinaoneka tofauti na miaka ya nyuma iliyopita hakukuwa na nguzo hata moja hivyo endeleeni kuwa na uvumilivu ili tuweze kumalizia changamoto zilizopo na ahadi zake.

Ilani ya chama cha mapinduzi CCM inaelekeza kuwa maeneo yote ambayo hayajafikiwa na umeme yafikiwe ili wananchi wa maeneo husika waweze kuondokana na giza na wakae kwenye mwanga.

Chanzo: fullshangwe