Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichokisema Bashiru Ally baada ya majibu ya Membe

29835 MEMBEE+PIC Bernard Membe, Waziri Mstaafu na Mjumbe wa CCM

Mon, 3 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ni vita mpya kati ya Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally na Bernard Membe.

Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na Dk Bashiru kutumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuhoji kitendo cha kusambaa kwa ujumbe katika mitandao ya kijamii ulioandikwa na mtu aliyejiita Bernard Membe, akijibu wito wa katibu mkuu huyo.

Juzi Desemba Mosi, 2018 Dk Bashiru alirejea kumtaka Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kwenda ofisini kwake, akidai mbunge huyo wa zamani wa Mtama anatuhumiwa kuandaa mpango wa kumkwamisha Rais John Magufuli katika uchaguzi wa Rais, kwamba lengo la wito wake huo ni kumueleza kama anayoyasikia ni kweli au si kweli.

Katika kile kinachoonekana kuwa majibu ya mtu anayejiita Membe katika mitandao ya kijamii baada ya wito huo wa Dk Bashiru yamemtibua katibu mkuu huyo, kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter amesema;

“Nakuita ofisini unanijibu Twitter na kunipa masharti. Ninapokuita nafanya hivyo kama Katibu Mkuu wa chama chako. Kama wewe si mwanachama ni vyema ukasema rasmi,” amesema Dk Bashiru kupitia ukurasa wake huo.

Katika majibu ya wito huo, mtu anayejiita Membe amesema amempelekea Dk Bashiru ujumbe wa kukubali kumuona mara atakaporejea Tanzania kutoka nje ya nchi.

Amesema ameshangazwa na utaratibu uliotumika kumuita, lakini kwa sababu ya ugeni kazini na kwa sababu anamheshimu (Dk Bashiru) atakwenda kumuona ofisini kwake.

Katika ujumbe huo, ‘Membe’ huyo anasema atakapokwenda ofisini kwa Dk Bashiru, mtu anayemtuhumu kuandaa mkakati wa kumng’oa Rais Magufuli, naye awepo ili kuthibitisha tuhuma hizo.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz