Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akina Mdee warudi kortini

A3381e19ed342fdd55acd81776269861.jpeg Akina Mdee warudi kortini

Sat, 25 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee na wenzake 18 wamefungua upya kesi ya kupinga uamuzi wa kuvuliwa uanachama.

Wamefikia hatua hiyo baada ya kufanya marekebisho waliyoambiwa wayafanye katika maombi ya awali yaliyotupwa Juni 22, 2022 na Jaji Mfawidhi John Mgeta.

Wakili wa wabunge hao, Aliko Mwamanenge alibainisha hayo alipozungumza na gazeti hili jana na kusema kuwa tayari wameshapeleka maombi hayo mahakamani yakiwa na marekebisho husika pamoja na maombi ya kutaka zuio la mahakama ili waendelee na hadhi ya ubunge wao mpaka uamuzi wa kesi hiyo utakapotolewa.

“Tulishawasilisha maombi hayo tangu Juni 23, tunachosubiri ni wito wa mahakama na kupangiwa Jaji,” alisema. Alisema tayari wabunge hao wameshamwandikia Spika wa Bunge kumfahamisha kwamba wameshawasilisha kesi mpya mahakamani. Katika maombi yao, Mdee na wenzake walikuwa wakiomba kibali cha kufungua kesi dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live