Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akina Dk. Slaa wataka uchaguzi serikali mitaa usogezwe mbele

Tr Slaa Mwamakula Akina Dk. Slaa wataka uchaguzi serikali mitaa usogezwe mbele

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Sauti ya Watanzania imeshauri uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwaka huu, usogezwe mbele hadi uchaguzi mkuu wa 2025, ili kupata muda wa kukamilisha mchakato wa upatikanaji katiba mpya. 

Wito huo umetolewa na taasisi hiyo wakati wajumbe wake, akiwemo Dkt. Wilbroad Slaa, Askofu Emmaus Mwamakula na Wakili Boniface Mwabukusi, wanazungumza na waandishi wa habari leo tarehe 8 Januari 2024, jijini Dar es Salaam, kuhusu miswada ya marekebisho ya uchaguzi iliyowasilishwa bungeni mwaka jana.

Wakili Mwabukusi amedai kuwa muda wa kukamilisha mchakato huo unatosha kwa kuwa kazi kubwa ilishafanyika na kwamba zoezi hilo linaweza kufanyika ndani ya miezi mitatu.

“Kwa kuwa jambo si gumu sababu asilimia kubwa ya wale watu walioshiriki kukusanya maoni ya wananchi wapo na wengine wapya wapo, utengenezwe utaratibu wa sheria ihuishwe na kwa kuisoma hii katiba yetu Rais ana mamlaka wanaweza kusogeza mbele uchaguzi wa serikali za mitaa ili uchaguzi wote ufanyike pamoja mwakani na hilo linawezekana.

“Kinachotakiwa sasa ni utungwaji wa sheria kukwamua pale Mzee Warioba alivyopigwa sarakasi bunge la katiba likakusanya maoni ikaja katiba pendekezwa, pale ndipo penye mkwamo na hiyo kazi ukiwapa watu makini wenye uchungu na nchii inahitaji miezi mitatu tu kuunganisha maeneo gani yenye shida,” amesema Mwabukusi.

Wakili Mwabukusi amedai kuwa, katiba ya sasa haihitaji marekebisho madogo kwa kuwa ina viraka zaidi ya 14 hivyo inapaswa kuandikwa upya, huku akidai inatakiwa katiba mpya iwabane viongozi kuwatumikia wananchi wanaowachagua.

Kwa upande wake Askofu Mwamakula, amesema kwa sasa Bunge limebeba dhamana ya kufanyia kazi maoni na mapendekezo ya wananchi yaliyoachwa, kwa kuhakikisha yanajumuishwa ili sheria zitakazotungwa zikidhi matakwa yao.

“Miswada iko chini ya kamati ya bunge, ina wajibu mkubwa kusikiliza maoni hayo, kuyachambua na kuangalia yale yenye maslahi mapana kwa taifa wayachukue.

"Nafasi ipo kwa wabunge kuhakikisha kile kinachopita ni maoni ya wananchi lakini serikali ina nafasi kama imeona kuna namna yoyote huwezi kurekebisha wanayo nafasi ya kuiondoa bungeni waiandae upya,” amesema Askofu Mwamakula.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live