Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aishiwa nguvu ghafla kwenye maandamano

Aishiwa Nguvu Aishiwa nguvu ghafla kwenye maandamano

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: Mwananchi

Mtu mmoja ambaye jina lake halijafahamika ameishiwa nguvu wakati maandamano ya wafuasi wa Chadema yakiendelea kuelekea ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo Barabara ya Sum Nujoma jijini Dar es Salaam leo Januari 24, 2024.

Mtu huyo alipoteza nguvu na kusaidiwa na waandamanaji wenzake waliokuwa pamoja naye na kumpeleka kivulini kisha kumlaza na kuanza kumpepea.

Maandamano hayo tayari yamefika ofisi za UN ambapo viongozi wa Chadema wameingia ndani kuwasilisha barua yenye ujumbe wanaoukusudia.

Chanzo: Mwananchi