Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahadi za Sungusia zawakuna wajumbe TLS

Wakili Harold Sungusia.jpeg Ahadi za Sungusia zawakuna wajumbe TLS

Sun, 14 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais mpya wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Harold Sungusia ameahidi kuwa taasisi hiyo itakuwa kiungo kizuri kati ya Serikali na wananchi katika mchakato wa kuandika katiba mpya pamoja na kurekebisha sheria dhaifu zilizopitwa na wakati nchini.

Rais mpya wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Harold Sungusia ameahidi kuwa taasisi hiyo itakuwa kiungo kizuri kati ya Serikali na wananchi katika mchakato wa kuandika katiba mpya pamoja na kurekebisha sheria dhaifu zilizopitwa na wakati nchini. Rais Sungusia amesema kuwa watakuwa mstari wa mbele kuisaidia Serikali kurekebisha vipengele vyote dhaifu vya sheria katika kuhakikisha kuwa taifa linapata katiba nzuri na vile vile chama hicho kitafanya jitihada za kuwashirikisha wananchi katika uandaaji wa sheria hizo. Akizungumza leo Jumamosi Mei 13, 2023 mara baada kuapishwa rasmi kushika wadhifa huo wa Urais kwa muda wa mwaka mmoja, Wakili Sungusia pia ameelezea kuridhishwa na uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano, Arusha (AICC) akisema kuwa ulizingatia taratibu zote za kidemokrasia ikiwemo haki na usawa. Katika uchaguzi huo, Wakili Sungusia aliibuka mshindi wa Urais wa TLS bada ya kupata idadi ya Kura 748 kati ya kura 825 zilizopigwa, huku akimuacha mbali mpinzani wake Reginald Shririma aliyepata kura 77. Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TLS, Wakili Mwandamizi Charles Rwechungura pia alimtangaza Wakili Aisha Sinda kuwa mshindi wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Chama Cha hicho. Aisha alipata kura 527 dhidi ya kura 261 za Emmanuel Agostino huku Revocatus Kuuli akipata kura 32. Akuzungumzia matokeo hayo, Wakili Fauziyat Mustapha amesema kuwa wana Imani kubwa na viongozi waliochaguliwa na kwamba watashirikiana nao katika kulinda maadili ya taaluma hiyo, ikiwemo kupambana na vitendo vya rushwa. "Sisi ndio tumewachagua na mimi binafsi nimeridhika na matokeo, ila peke yao hawawezi hivyo tutatoa kila ushirikiano watakaoutaka kwetu katika kuhakikisha waatekeleza majukumu yao sambamba kulinda na kutetea maslahi ya taaluma yetu" amesema Uchaguzi huo ulitanguliwa na mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Mawakili Tanganyika uliofunguliwa na Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango ambaye aliuagiza uongozi wa TLS kushughulikia tatizo la baadhi ya wanasheria wanaokiuka maadili ya kazi zao kwa kuendekeza vitendo vya rushwa. Akizungumzia maelekezo hayo ya Dk Mpango, Rais wa TLS amesema watashirikiana kudhibiti vitendo vyote vya rushwa katika taaluma yao na kusisitiza kuwa chama hicho pia kinaendelea na mkakati wa kuboresha taaluma ya sheria nchini pamoja na kushughulikia maslahi ya wanachama wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live