Aziza Ally aapishwa rasmi kuwa Mbunge, baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kumteua kuwa Mbunge wa Viti Maalum, jambo ambalo linamrejesha mjengoni baada ya kukaa nje kwa takribani miaka 13,
Aziza anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bahati Ndingo, aliyejiuzulu nafasi hiyo baada ya kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mdogo wa kuwania kiti cha ubunge Jimbo la Mbalali.
Bahati alijiuzulu nafasi hiyo baada ya kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mdogo wa kuwania kiti cha ubunge Jimbo la Mbalali.
Uchaguzi ambao ulifanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Francis Mtega, kilichotokea Julai Mosi, 2023 kwa ajali ya kugongwa na trekta dogo (power tiller).
Septemba 20, 2023; Msimamizi wa uchaguzi mdogo wa hilo, Missana Kwangura alimtangaza Bahati kuwa mshindi wa katika uchaguzi huo mdogo, ambapo alipata kura 44, 334 dhidi ya mshindani wake wa karibu, Modestus Kilufi wa ACT - Wazalendo, aliyepata kura 10, 014.